• HABARI MPYA

  Friday, September 21, 2018

  KMC YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU, YAWACHAPA STAND UNITED 2-0 DAR

  Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) leo imepata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuilaza 2-0 Stand United Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa wafungaji wa mabao hayo Abdallah Masoud ‘Cabaye’ dakika ya nane na Emmanuel Mvuyekule dakika 45 na sasa KMC inafikisha pointi sita katika mechi yake ya tano, nne za awali tatu ikitoa sare na moja ikifungwa.
  Stand United walicheza ovyo kipindi cha kwanza na kuwaruhusu wenyeji kupata mabao mawili katika kipindi cha kwanza, lakini kipindi cha pili wakabadilika hata hivyo hawakufanikiwa kukomboa mabao.

  Stand United wanabaki na pointi zao sita baada ya kucheza mechi tano, leo wakifungwa kwa mara ya tatu na nyingine mbili wameshinda.
  Kikosi cha KMC kilikuwa; Juma Kaseja, Aaron Lulambo, Ally Ramadhani, Ally Ally, Ally Msengi, Rayman Mgungila, Abdallah Masoud ‘Cabaye’, George Sengija, Sadallah Lipangile, Emmanuel Mvuyekuye na Cliff Anthony/Hassan Kabunda dk55.
  Stand United; Mohammed Makaka, Niyonkuru Nassor, Bigirimana Ramadhani, Erick Murilo, Ndoriyobija Erick, Erick Mbirizi/ Charles Chinonso dk70, Bigirimana Blaise, Jackob Masawe, Alex Kitenge, Hafidh Mussa na Sextus Sabilo/Datius Peter dk76.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU, YAWACHAPA STAND UNITED 2-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top