• HABARI MPYA

  Wednesday, September 26, 2018

  MOURINHO AMVUA UNAHODHA POGBA BAADA YA KUMUAMBIA ANAKWENDA BARCELONA

  Paul Pogba amevuliwa che Nahodha Msaidizi wa Manchester United baada ya kumuambia Jose Mourinho anataka kuhamia Barcelona 


  TAKWIMU ZA PAUL POGBA MSIMU WA 2018-19 HADI SASA

  Mechi: 7
  Mabao: 4
  Pasi za mabao: 2 
  Kadi za njano: 0 
  KIUNGO Paul Pogba amevuliwa che Nahodha Msaidizi wa Manchester United baada ya kumuambia kocha wake, Jose Mourinho anataka kuhamia Barcelona.
  Nyota huyo wa Ufaransa ameifungia mabao matatu United msimu huu, lakini Mourinho anaamini haikubaliki kwa mchezaji anayeshinikiza kuondoka kuendelea kuvaa beji ya Unahodha.
  Kikosi kiliambiwa uamuzi huo katika Uwanja wa mazoezi wa Carrington saa chache kabla ya mechi ya Carabao Cup ambayo United ilifungwa kwa penalti 8-7 na Derby County, Pogba akiushuhudia mchezo huo kutoka jukwaani.
  "Ukweli ni kwamba nimefanya uamuzi huu kwa Paul, hatakuwa Nahodha Msaidizi tena,"amesema Mourinho. "Ni mimi yule yule niliyempa Paul Unahodha Msaidizi. Hakuna ugomvi kabisa, uamuzi tu na sihitaji kufafanua,". 
  Pogba aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 89 kutoka Juventus, amemuambia Jose Mourinho kwamba anataka kuondoka Manchester United katika jitihada zake za kushinikiza uhamisho wa kwenda Barcelona.
  Uhusiano wa Mourinho na Pogba mwenye umri wa miaka 25 uliharibika miezi 18 iliyopita na inafahamika wawili hao wamekuwa wakiwasiliana kwa ujumbe wa maandishi kwenye simu wiki za karibuni, ingawa tetesi za mchezaji huyo kuondoka Manchester zimezidi kuongezeka.
  Tayari Pogba amemuambia Makamu Mwenyekiti wa Old Trafford, Ed Woodward nia yake ya kuondoka baada ya wakala wake, Mino Raiola kukamilisha dili na Barcelona juu ya maslahi binafsi.
  Woodward bado anataka kumbakiza nyota huyo mkubwa wa timu, lakini uamuzi wa Mourinho kumshusha wadhifa mchezaji huyo utafanya hilo liwe gumu sasa.
  Nidhamu ya Pogba pia imekuwa tatizo lingine kwa Mourinho na Wasaidizi wake pia.
  Hawakufurahishwa na kitendo cha mchezaji huyo kupiga muziki kwa sauti kubwa kwenye basi la timu wakati ilipokuwa inakwenda kwenye mechi na Wolves Jumamosi Uwanja wa Old Trafford, wakiamini walipaswa kuwa kimya wakitafakari mechi.
  Pogba pia anashutumiwa kwa ubinafsi baada ya kutumia gari lake, Rolls-Royce kwa safari za kambini na aliendesha kutoka Burnley hadi Uwanja wa Ndege kujiunga na kikosi cha Ufaransa baada ya United kushinda Uwanja wa Turf Moor mapema mwezi huu, wakati wachezaji wenzake wote kwenye timu walikwenda kwa basi la klabu.
  Wakati inafahamika wazi uhusiano wa Mourinho na Pogba si mzuri tena, bado maneno ya mchezaji huyo nayo yamekuwa tatizo pia United. 
  Mwezi uliopita alisema hawezi kuzungumzia hali yake ndani ya klabu kwa woga wa kutozwa faini, na aliwahi kuponda mfumo wa Mourinho akitaka timu icheza kwa kushambulia baada ya sare na Wolves.
  "Hapo ni Old Trafford," alisema. "Tupo hapa kushambulia. Timu zinaogopa zinapoona Man United inashambulia na kushambulia. Hilo ndilo kosa letu leo. Tulishinda 1-0 hivyo ilikuwa nzuri kwetu. Kisha tukaanza kupaki basi na kushambulia kwa kushitukiza. Tuliacha kucheza kwa kushambulia kama tulivyofanya kipindi cha kwanza na hatukuwatia matatizoni haswa.
  "Tupo Old Trafford na tunapaswa kushambulia na kusukuma kama tulivyofanya dhidi ya Tottenham, Liverpool, Chelsea na Arsenal msimu uliopita. Tunapocheza hivi ni rahisi,".' 
  Mourinho alikasirika baada ya mechi na Wolves na alikuwa akiwalaumu wachezaji wake Jumatatu na Jumanne mazoezini.
  Katika mazoezi ya Jumanne usiku, alisema sare ya 1-1 ni somo muhimu, somo linalojirudia kila wiki, somo ambalo wavulana wengine hawajifunzi. Kila timu inayocheza na Man Utd inachezaji kwa bidii. Tunahjitaji kufanya kama wao, motisha na tamaa, kwa asilimia 95 haitoshi,".'
  Mourinho alimpa Pogba siku mbili za mapumziko baada ya mchezo huo na akampumzisha kwenye mchezo wa jana huku  Ashley Young akipewa beji ya Unahodha wa klabu.
  Lakini ni wazi kwamba uhusiano wa wawili hao umeharibika na kitendo cha Mourinho kumvua mchezaji huyo Unahodha ni kilelezo tosha.
  Pogba amegunga mabao manne kwenye saba msimu huuu — matatu kwa penalti — lakini haijabadili mawazo yake ya kuondoka United miaka miwili tangu ajiunge nayo tena kutoka Juventus kwa dau la rekodi ya dunia wakati huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOURINHO AMVUA UNAHODHA POGBA BAADA YA KUMUAMBIA ANAKWENDA BARCELONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top