• HABARI MPYA

  Thursday, September 27, 2018

  YANGA SC KUENDELEA KUWAKOSA JUMA WOTE, ABDUL NA MAHADHI MECHI NA SIMBA JUMAPILI TAIFA

  Na Doreen Mkude, MOROGORO
  YANGA SC itaendelea kuwakosa beki Juma Abdul na kiungo Juma Mahadhi kuelekea mchezo wa Jumapili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao, Simba SC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Akizungumza mjini Morogoro leo, Meneja wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kwamba wachezaji hao bado ni majeruhi na hawapo tayari kwa mchezo wa Jumapili.
  Pamoja na hayo, Meneja huyo na mchezaji wa klabu tangu mwaka 2006 hadi Mei mwaka huu alipostaafu na kuhamia kwenye benchi la Ufundi, amesema kwamba anaamini kila mchezaji atakayepewa nafasi siku ya Jumapili atafanya vizuri.

  Beki wa Yanga, Juma Abdul hatakuwepo kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya mahasimu, Simba SC Uwanja wa Taifa 

  Amesema hata mechi iliyopita klabu iliwakosa wachezaji wake wa kikosi cha kwanza beki Kelvin Yondan, kiungo Mrisho Ngassa na mshambuliaji Mkongo Heritier Makambo, lakini waliocheza wakaleta ushindi wa 2-0 dhidi ya Singida United.
  “Tumekuja Morogoro sehemu ambayo ni tulivu na mazoezi tunaendelea vizuri, kila mchezaji ana ari ya mchezo siku ya Jumapili. Kwetu sisi tumejipanga vizuri kwa ajili ya mchezo wa Jumapili na kuweza kupata pointi tatu,”amesema.
  Yanga SC wameweka kambi mjini Morogoro wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Jamhuri kujiandaa na mchezo wa Jumapili, ambao utakuwa wa tano kwao wa Ligi Kuu msimu huu baada ya kushinda yote minne yote ya awali.
  Watani wao, Simba SC wamebaki Dar es Salaam katika hoteli ya Sea Scape, Kunduchi huku wakiendelea na mazoezi Uwanja wa Boko Veterani. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC KUENDELEA KUWAKOSA JUMA WOTE, ABDUL NA MAHADHI MECHI NA SIMBA JUMAPILI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top