• HABARI MPYA

  Monday, September 24, 2018

  AISHI MANULA AFIKISHA MECHI 50 SIMBA SC, AMEFUNGWA MABAO 24 ANA ‘CLEAN SHEETS’ 32

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIPA Aishi Manula jana amedaka mechi yake ya 50 Simba SC tangu asajiliwe kutoka Azam FC Julai mwaka jana huku akifungwa bao la 24. 
  Simba SC ilipata ushindi wa kwanza katika mechi tatu jana, baada ya kuichaoa 3-1 Mwadui FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga ikitoka kucheza mechi mbili zilizopita bila kushinda, ikitoa sare ya 0-0 na Ndanda FC mjini Mtwara na kufungwa 1-0 na Mbao FC mjini Mwanza.
  Bahati mbaya kwa Wekundu hao wa Msimbazi walimpoteza Nahodha wao, aliyetolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 80 baada ya kumpiga ngumi beki wa Mwadui FC, Revocatus Richard wakati wawili hao wakigombea mpira.
  Ushindi wa jana unaifanya Simba SC ifikishe pointi 10 baada ya kucheza mechi tano kuelekea pambano dhidi ya watani wa jadi, Yanga Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Aishi Manula jana amedaka mechi yake ya 50 Simba SC tangu asajiliwe kutoka Azam FC  

  Lakini aliondoka uwanjani akiwa amekwishaifungia Simba mabao mawili, la kwanza kwa penalti dakika ya 41 baada ya kiungo Shiza Kichuya kuangushwa na Miraj Maka kwenye boksi dakika ya 40 na la pili dakika ya 45, akimalizia pasi ya beki wa kulia, Shomari Kapombe, hivyo kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 100 kwenye Ligi Kuu tangu imeanzishwa mwaka 1996.
  Bao la tatu la Simba SC lilifungwa na Kagere dakika ya 50 kwa shuti kali kutoka umbali wa mita 16, wakati la Mwadui FC lilifungwa na Charles Ilamfya dakika ya 81 baada ya kumzidi mbio na ujanja, beki Muivory Coast, Serge Wawa Pascal.
  Kwa Aishi, jana aliruhusu bao la 24 tu tangu ameanza kulinda lango la Simba SC, huku akiwa ana rekodi ta kudaka mechi 32 kuelekea pambano dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga SC Jumapili. 
  Aishi Manula amedaka mechi 32 bila kuruhusu bao kati ya 50 alizocheza Simba SC

  REKODI YA AISHI MANULA SIMBA
  1. Simba 1-0 Rayon Sport (Hakufungwa Kirafiki Simba Day Taifa)
  2. Simba 0-0 Mlandege FC  (Hakufungwa Kirafiki Amaan, Zbar)
  3. Simba 0-0 (5-4 penalti) Yanga (Hakufungwa Ngao ya Jamii, Taifa Penalti)
  4. Simba 7 – 0 Ruvu Shooting (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
  5. Simba 0 – 0 Azam FC (Hakufungwa Ligi Kuu Chamazi)
  6. Simba 3 – 0 Mwadui (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
  7. Simba 2 – 2 Mbao FC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Kirumba, Mwanza)
  8. Simba 0-0 Milambo (Aliingia, hakufungwa Kirafiki A. Mwinyi, Tabora)
  9. Simba 2-1 Stand United (Alifungwa moja Ligi Kuu Shinyanga)
  10. Simba 1 – 1 Mtibwa Sugar (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
  11. Simba 4 – 0 Njombe Mji (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
  12. Simba 1-1 Yanga (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
  13. Simba 1-0 Mbeya City (Hakufungwa Ligi Kuu Sokoine)
  14. Simba 1-0 Tanzania Prisons (Hakufungwa Ligi Kuu Sokoine)
  15. Simba 1-1 Lipuli FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
  16. Simba 1-1 (Penalti 3-4) Green Warriors (Alifungwa moja na penalti nne Kombe la TFF Chamazi)
  17. Simba 2-0 Ndanda FC (Hakufungwa Ligi Kuu Nangwanda)
  18. Simba 4-0 Singida United  (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
  19. Simba 2-0 Kagera Sugar  (Hakufungwa Ligi Kuu Kaitaba)
  20. Simba 4-0 Maji Maji FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
  21. Simba 3-0 Ruvu Shooting FC (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
  22. Simba 1-0 Azam FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
  23. Simba 4-0 Gendarmerie Tnare  (Hakufungwa, Kombe la Shirikiaho Kuu Taifa)
  24. Simba 2-2 Mwadui FC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Kambarage)
  25. Simba 1-0 Gendarmerie Tnare  (Hakufungwa – Kombe la Shirikisho Djibouti)
  26. Simba 5-0 Mbao FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
  27. Simba 3-3 Stand United (Alifungwa zote tatu Ligi Kuu Taifa)
  28. Simba 2-2 Al Masry  (Alifungwa mbili moja kwa penalti Kombe la Shirikisho Taifa)
  29. Simba 0-0 Al Masry  (Hakufungwa Kombe la Shirikisho Port Said)
  30. Simba 2-0 Njombe Mji FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa Njombe)
  31. Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa) 
  32. Simba 3-1 Mbeya City  (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
  33. Simba 2-0 Tanzania Prisons  (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
  34. Simba 1-1 Lipuli FC  (Alifungwa moja, Ligi Kuu Samora)
  35. Simba 1-0 Yanga SC (Hakufungwa, Ligi Kuu Taifa)
  36. Simba 1-0 Ndanda FC  (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
  37. Simba 1-0 Singida United  (Hakufungwa Ligi Kuu Namfua)
  38. Simba 0-0 (3-2 Penalti) Kariobangi Sharks  (Hakufungwa, akaokoa penalty moja SportPesa SuperCup Nakuru)
  39. Simba 0-0 (5-4 Penalti) Kakamega Homeboys (Hakufungwa SportPesa SuperCup Nakuru)
  40. Simba 0-2 Gor Mahia (Alifungwa mbili SportPesa SuperCup Nakuru)
  41. Simba SC 1-1 F.C.E KSAIFA (ya Palestina, hakufungwa kirafiki ziara ya Uturuki)
  42. Simba SC 3-1 MC Oujder (ya Morocco, hakufungwa Kirafiki ziara ya Uturuki)
  43. Simba SC 1-1 Asante Kotoko (ya Ghana, alifungwa moja Kirafiki Simba Day Taifa)
  44. Simba SC 2-1 Arusha United (Alifungwa moja Kirafiki Uwanja wa S.A. Abeid, Arusha)
  45. Simba SC 2-1 Mtibwa Sugar (Alifungwa moja Ngao ya Jamii Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza)
  46. Simba SC 1-0 Tanzania Prisons (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
  47. Simba SC 2-0 Mbeya City (Hakufungwa, Ligi Kuu Taifa alitoka baada ya kuumia dk53 akaingia Ally Salim)
  48. Simba SC 0-0 Ndanda FC (hakufungwa Ligi Kuu Mtwara)
  49. Simba SC 0-1 Mbao FC (Alifungwa moja kwa penalti Ligi Kuu Mwanza)
  50. Simba SC 3-1 Mwadui FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Shinyanga)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AISHI MANULA AFIKISHA MECHI 50 SIMBA SC, AMEFUNGWA MABAO 24 ANA ‘CLEAN SHEETS’ 32 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top