• HABARI MPYA

  Saturday, September 29, 2018

  ALLIANCE FC YAZINDUKA YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU, YAICHAPA KMC 2-1 NYAMAGANA

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  TIMU ya Alliance FC imepata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuichaa KMC ya Kinondoni mjini Dar es Salaam mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
  Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, mabao ya Alliance FC yamefungwa na Dickson Ambundo dakika ya tano na Juhudi Philemon dakika ya 10, wakati la KMC limefungwa na Emmanuel Mvuyekure dakika ya 56.
  Alliance FC ambayo kama KMC zote zimepanda Ligi Kuu msimu huu, kwa ushindi huo inafikisha pointi nne baada ya kucheza saba, ikishinda moja na kutoa sare moja, huku nyingine tano ikifungwa zote. 
  Timu ya Alliance FC imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu leo mjini Mwanza

  KMC inayofundishwa na kocha Mrundi, Ettienne Ndayiragijje yenyewe inabaki na pointi zake saba baada ya kucheza mechi saba pia, ikishinda moja, sare nne na kufungwa mbili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALLIANCE FC YAZINDUKA YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU, YAICHAPA KMC 2-1 NYAMAGANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top