• HABARI MPYA

    Friday, January 16, 2026

    DODOMA JIJI NA SINGIDA BLACK STARS ZATOKA SARE 1-1 JAMHURI


    WENYEJI, Dodoma Jiji FC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na jirani zao, Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
    Mabao yote katika mchezo wa leo yamefungwa kwa penalti, Dodoma Jiji FC walitangulia kupitia kwa mshambuliaji, Yassin Mgaza dakika ya 83, kabla ya kiungo Mtogo, Marouf Tchakei kuisawazishia Singida Black Stars dakika ya 90’+6.
    Kwa matokeo hayo, Singida Black Stars inafikisha pointi tisa katika mchezo wa sita nafasi ya 11, wakati Dodoma Jiji FC inafikisha pointi saba katika mchezo wa tisa pia nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DODOMA JIJI NA SINGIDA BLACK STARS ZATOKA SARE 1-1 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top