• HABARI MPYA

  Thursday, September 27, 2018

  MBONDE AIPELEKA MTIBWA SUGAR KILELENI LIGI KUU, RUVU SHOOTING WAPATA USHINDI WA KWANZA MECHI YA SITA

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  TIMU za Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting leo zimetumia vyema viwanja vya nyumbani kwa kupata ushindi, japo mwembamba zote 1-0 dhidi ya wapinzani wao, Mwadui FC na Ruvu Shooting katoka mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, bao pekee la mshambuliaji Stahmili Mbonde dakika ya 28 lilitosha kuwapa pointi zote tatu wenyeji, Mtibwa Sugar dhidi ya Mwadui FC.
  Na Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, bao pekee la Said Mussa dakika ya 50 lilitosha kuwapa wenyeji Ruvu Shooting ushindi wa 1-0 dhidi ya African Lyon.

  Stahmili Mbonde akishangilia baada ya kufunga bao pekee leo Mtibwa Sugar ikiilaza 1-0 Mwadui FC

  Mechi kati ya Stand United na Tanzania Prisons iliyokuwa ifanyike leo pia Uwanja wa CCM kambarage mjini Shinyanga imesogezwa mbele hadi kesho.
  Kwa ushindi wa leo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi saba na kuifikia Mbao FC kileleni ambayo ina mechi moja mkononi.
  Ruvu Shooting yenyewe huu ni ushindi wao wa kwanza katika mechi sita, baada ya kufungwa tatu awali na sare mbili, hivyo wanafikisha pointi tano, ingawa wanabaki nafasi ya 18 katika Ligi Kuu ya timu 20 mbele ya Mwadui wenye pointi mbili na Alliance FC pointi moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBONDE AIPELEKA MTIBWA SUGAR KILELENI LIGI KUU, RUVU SHOOTING WAPATA USHINDI WA KWANZA MECHI YA SITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top