• HABARI MPYA

  Friday, September 21, 2018

  NTALE WA PANGANI NDIYE MSHINDI WA DROO YA KWANZA YA PROMOSHENI YA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  DEREVA Bodaboda mkazi wa Mwera, Pangani, Ntale Lusalula Rajabu (21) ameweka rekodi kwa kufungua dimba na kuwa mshindi wa kwanza kwa kushinda bajaji mpya kutoka SportPesa.
  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumtangaza mshindi huyo Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas alisema “Kupitia promosheni ya kwanza kuliyoifanya mwaka jana tulitoa bajaji 100 na tumekuwa tukiwafatilia washindi wetu na kusema ukweli masiha yao si ya kuigiza tena, ni maisha halisi, bora zaidi na wanawe kujikimu kimaisha mfano waliokuwa wanapitia changamoto ya kuwapeleka watoto shuleni kutokana na ada ama vifaa vya shule wamefanikisha hilo, na waliokuwa wanapata changamoto kuendesha familia zao kwa sasa wanaendelea vizuri.” 

  Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas (kulia) akiwa na Ntale Lusalula Rajabu

  “Baada ya sisi kuona kwamba tumewasaidia familia zaidi ya 100 na Tanzania tunaishi familia nyingi tumeona turudishe tena shindano kama hili ili na leo tumefanya droo ya kwanza na mshindi ametoka sehemu za Mwera Mkoa wa Tanga wilaya ya Pangani. Hii maana yake ni kwamba wanaoshiriki kucheza na SportPesa ambapo pia ni burudani”
  “Hii inatutia moyo sisi kama kampuni kwamba promosheni yetu inasikika na inajulikana sehemu kubwa ya nchi na watu wa aina tofauti na hata washindi tuliowapata kwenye promosheni iliyopita asilimia kubwa walipatikana kutoka mikoani”
  “Safari hii mteja wa SportPesa anapaswa kuweka ubashiri wake na moja kwa moja ataingia kwenye droo ya kuwania bajaji mpya”.
  Mtumiaji wa mitandao yoyote ya simu anaweza kucheza kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupiga *150*87# kwa USSD, APP, njia ya mtandao(WEBSITE) na kupitia ujumbe mfupi yaani SMS.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NTALE WA PANGANI NDIYE MSHINDI WA DROO YA KWANZA YA PROMOSHENI YA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top