• HABARI MPYA

  Friday, September 28, 2018

  SPORTPESA WAMKABIDHI ABDALLAH SELEMAN ALLY WA MBAGALA BAJAJI YAKE MPYA

  HATIMAYE mshindi wa pili wa bajaj mpya kutoka SportPesa, Abdallah Seleman Ally, mkazi wa Mbagala, amekabidhiwa bajaj yake mpya katika hafla fupi iliyofanyika Mbagala Zakhem jijini Dar es salaam. 
  Akikabidhi bajaj hiyo kwa mshindi, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa kampuni ya SportPesa, Tarimba Abbas, alisema hii ni uthibitisho kwamba kampuni hiyo inatekeleza ilichoahidi. 
  "Kubashiri na SportPesa siyo mauza uza au mazingaombwe, ni kitu cha kweli na halisi, na ndiyo maana tuko hapa ili kuthibitisha kwamba mchezo huu ni halisi" Alisema Tarimba. 
  "Bajaj hizi zipo mia moja na kila atakayebashiri anaingia moja kwa moja kwenye kwenye droo na anaweza kujishindia bajaj kama huyu kijana tunayemkabidhi leo" Aliongeza mkurugenzi huyo.

  Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas (kulia) akimkabidhi funguo Abdallah Seleman Ally leo Mbagala Zakhem

  Naye Abdallah Seleman, aliyejishindia bajaj kutoka SportPesa alisema, anaamini kwamba atatimiza ndoto zake baada ya kufanikiwa kushinda Bajaj hiyo. 
  "Naamini bajaj hii itanisaidia kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zinanikabili, sasa naamini kwamba kupitia bajaj hii nitafanikisha malengo" Alisema mshindi huyo. 
  Wakati huo huo Kassim Mohammed ambaye ni rafiki wa karibu wa Abdallah Selemani, mshindi wa pili wa Bajaj kutoka Mbagala alieleza furaha yake kwa kwa namna ambavyo rafiki yake ameweza kushinda.
  "Nimefurahi kwakuwa mimi ndiye niliyemshawishi kubashiri na SportPesa na baada ya kunipa taarifa ya ushindi wake nilifurahi sana" Alisema Kassim
  Pia rafiki huyo alisema kwa kitendo cha ushindi na hatimaye kukabidhiwa Bajaj hiyo kimemfanya aamini kwamba sportpesa haina ubabaishaji, na aliahidi kuendelea kubashiri na SportPesa
  SportPesa inaendelea na promosheni yake ya Shinda Zaidi na SportPesa, itakayodumu kwa siku mia moja huku washindi mia moja wakitarajiwa kushinda katika promosheni hiyo. 
  Katika awamu hii ya promosheni, SportPesa imewarahisishia wateja wake kwa kuweka menu rahisi ya kubofya *150*87# ambayo kupitia menu hiyo mteja anaweza kufanya kila kitu kama kujisajili, kuweka fedha, kuweka ubashiri nk
  Watu wengi wameonekana kuhamasika kucheza na SportPesa hasa baada ya kurahisishiwa namna ya kucheza na uwepo wa promosheni ya kujishindia BajajI.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SPORTPESA WAMKABIDHI ABDALLAH SELEMAN ALLY WA MBAGALA BAJAJI YAKE MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top