• HABARI MPYA

  Sunday, September 30, 2018

  KASEJA ASEMA KMC WANAELEKEZA NGUVU ZAO KWENYE MCHEZO UJAO NA KAGERA SUGAR

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  KIPA mkongwe wa KMC, Juma Kaseja amesema kwamba wanaelekeza nguvu zao kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar Oktoba 2, Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Hiyo ni baada ya kupoteza mchezo wao uliopita jana kwa kufungwa 2-1 na wenyeji, Alliance FC Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
  “Tumemaliza mechi na Alliance FC, tunaondoka Mwanza, tunakwenda Bukoba. Sasa hivi akili zetu tunazielekeza kwenye mchezo ujao dhidi ya Kagera Sugar. Ni mechi ngumu hiyo, hatuhitaji kuendelea kupoteza mechi,”amesema.

  Juma Kaseja amesema wanaelekeza nguvu zao kwenye mechi na Kagera Sugar Oktoba 2

  Kaseja amesema kwamba kocha wao, Mrundi Ettienne Ndayiragijje ameona makosa yaliyojitokeza kwenye mechi na Alliance na atayafanyia kazi kabla ya mechi na Kagera Sugar.
  “Nina imani kubwa na hii timu huko mbele itafanya vizuri na kushangaza watu, kwa sababu ina wachezaji vijana wanaoendelea kuimarika kila siku,”amesema.
  Kwa sasa, KMC inashika nafasi ya 11 kwa pointi zake saba baada ya kucheza mechi saba, wakati wapinzani wao wajao, Kagera Sugar wana pointi saba za mechi sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KASEJA ASEMA KMC WANAELEKEZA NGUVU ZAO KWENYE MCHEZO UJAO NA KAGERA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top