• HABARI MPYA

  Saturday, September 29, 2018

  SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI ‘SIMBA DAMU’ MGENI RASMI KESHO MECHI YA WATANI WA JADI TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kesho katika mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Ndugai, mnazi wa Simba SC kuwa mgeni rasmi katika mchezo huo wa Ligi Kuu baina ya watani wa jadi.
  Ikumbukwe mechi hiyo itachezeshwa na refa Jeonisya Rukyaa kutoka Kagera akisaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Mohamed Mkono wa Dar es Salaam pembezoni mwa Uwanja na Mezani atakuwepo Elly Sasii.

  Spika Job Ndugai atakuwa mgeni rasmi kesho katika mechi ya watani wa jadi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam

  Jeonesia Rukyaa, refa wa Kagera tayari ana uzoefu wa kupuliza kipyenga katika michezo ya watani wa jadi, baada ya awali kuchezesha mechi mbili.
  Kwanza ilikuwa Desemba 13, mwaka 2014 mechi ya Mtani Jembe, Simba SC wakishinda 2-0, mabao ya Awadh Juma na Elias Maguri na ya pili Februari 20, mwaka 2016 Yanga SC wakishinda 2-0, mabao ya Donald Ngoma na Amissi Tambwe. 
  Mchezo wa kesho utakuwa wa pili kuzikutanisha timu hizo mwaka huu, baada ya Aprili 29 Simba SC kushinda 1-0, bao pekee la Erasto Edward Nyoni dakika ya 37, mechi ya marudiano ya msimu uliopita wa Ligi Kuu. 
  Mechi ya kwanza ya msimu huo, timu hizo zilitoka sare ya 1-1 Oktoba 28 Uwanja wa Taifa Simba wakitangulia kwa bao la Shiza Kichuya dakika ya 57, kabla ya Obrey Chirwa kuisawazishia Yanga dakika ya 60. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI ‘SIMBA DAMU’ MGENI RASMI KESHO MECHI YA WATANI WA JADI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top