• HABARI MPYA

  Sunday, September 30, 2018

  ZAHERA AMSIMAMISHA MAKAMBO KAMA MSHAMBULIAJI PEKEE YANGA SC MECHI NA SIMBA LEO

  Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga SC, Mwinyi Zahera amemuanzisha Mkongo mwenzake, Heritier Makambo kama mshambuliaji pekee kwa ajili ya mpambano dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba SC unaotarajiwa kuanza Saa 11:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.  
  Lakini amemuwekea viungo wanne, ambao ni Dues Kaseke, Mkongo mwingine Papy Kabamba Tshishimbi, Feisal Salum na Ibrahim Ajib.
  Kwa ujumla kikosi cha Yanga SC kinachoanza leo ni; Beno Kakolanya, Paulo Godfrey, Gardiel Michael, Kelvin Yondani, Abdallah Shaibu 'Ninja', Dues Kaseke, Papy Kabamba Tshishimbi, Haritier Makambo, Feisal Salum na Ibrahim Ajib.
  Katika benchi wapo; Klaus Kindoki, Amissi Tambwe, Mwinyi Hajji Mngwali, Raphael Daudi, Mrisho Ngassa na Matheo Anthony. 

  Heritier Makambo leo anasimama kama mshambuliaji pekee mechi dhidi ya Simba SC 

  Kwa upande wa mahasimu wao, Simba SC kikosi ni; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, James Kotei, Jonas Mkude, Cletus Chama, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya.
  Katika benchi wapo Deo Mushi ‘Dida’, Paul Bukaba, Asante Kwasi, Said Ndemla, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Nicholas Gyan na Adam Salamba.  
  Ikumbukwe mechi hiyo itachezeshwa na refa Jeonisya Rukyaa kutoka Kagera akisaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Mohamed Mkono wa Dar es Salaam pembezoni mwa Uwanja na Mezani atakuwepo Elly Sasii.
  Jeonesia Rukyaa, refa wa Kagera tayari ana uzoefu wa kupuliza kipyenga katika michezo ya watani wa jadi, baada ya awali kuchezesha mechi mbili.
  Kwanza ilikuwa Desemba 13, mwaka 2014 mechi ya Mtani Jembe, Simba SC wakishinda 2-0, mabao ya Awadh Juma na Elias Maguri na ya pili Februari 20, mwaka 2016 Yanga SC wakishinda 2-0, mabao ya Donald Ngoma na Amissi Tambwe. 
  Mchezo wa kesho utakuwa wa pili kuzikutanisha timu hizo mwaka huu, baada ya Aprili 29 Simba SC kushinda 1-0, bao pekee la Erasto Edward Nyoni dakika ya 37, mechi ya marudiano ya msimu uliopita wa Ligi Kuu. 
  Mechi ya kwanza ya msimu huo, timu hizo zilitoka sare ya 1-1 Oktoba 28 Uwanja wa Taifa Simba wakitangulia kwa bao la Shiza Kichuya dakika ya 57, kabla ya Obrey Chirwa kuisawazishia Yanga dakika ya 60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZAHERA AMSIMAMISHA MAKAMBO KAMA MSHAMBULIAJI PEKEE YANGA SC MECHI NA SIMBA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top