• HABARI MPYA

  Wednesday, September 26, 2018

  MANCHESTER UNITED YATOLEWA MAPEMAA KOMBE LA LIGI ENGLAND

  Kocha  wa Manchester United, Jose Mourinho akimfariji beki wake, Phil Jones baada ya kukosa penalti ya mwisho katika mchezo wa Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup wakitolewa kwa penalti 8-7 na Derby County ya kocha Frank Lampard iliyopo Championship baada ya sare ya 2-2 Uwanja wa Old Trafford jana.
  Mabao ya Man United yalifungwa na Juan Mata dakika ya tatu na Marouane Fellaini dakika ya tano ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90, wakati ya Derby yalifungwa na winga Harry Wilson anayecheza kwa mkopo kutoka Liverpool dakika ya 59 na Jack Marriott dakika ya 85.
  United ilimpoteza kipa wake, Sergio Romero aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 69 baada ya kudaka mpira nje ya boksi.
  Penalti za Derby zilifungwa na Mason Mount, Florian Jozefzoon, Harry Wilson, Jack Marriott, Bradley Johnson, Craig Bryson, Craig Forsyth na Richard Keogh, wakati za United zilifungwa na Romelu Lukaku, Ashely Young, Fellaini, Fred, Anthony Martial, Diogo Dalot na Nemanja Matic 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER UNITED YATOLEWA MAPEMAA KOMBE LA LIGI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top