• HABARI MPYA

  Sunday, September 02, 2018

  MCHEZAJI WA ATLETICO MADRID B AMNG'ATA WA REAL MADRID

  MECHI ya leo mahasimu wa Jiji la Madrid imeibua mshituko baada ya Nahodha wa Atletico, Tachi kumng'ata Vinicius Junior wa Real.
  Timu ya pili ya Atletico imeambulia pointi dhidi ya Real Madrid Castilla kwenye mechi ya Segunda Daraja B, lakini the hawakufurahishwa na matokeo hayo.
  Tukio hilo lilitokea baada ya Castilla kupata bao la kuongoza kufuatia mashambulizi mawili ya nguvu ya mchezaji mpya wa Los Blancos, Vinicius aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 38 msimu huu.

  Vinicius Junior aliuumwa na Nahodha wa Atletico Madrid B, Tachi leo kwenye mechi ya mahasimu ya Madrid 

  Mchezaji huyo Mbrazil mwenye umri wa miaka 18 alionyesha thamani yake kwa nini mabingwa wa Ulaya walitoa ada kubwa kumsajili yeye kwa kufunga bao zuri leo mchana akimtungua kipa wa Atletico, San Roman baada ya kuivuruga safu ya ulinzi.
  Lakini dakika tisa baadaye, Vinicius akaanguka na Nahodha wa Atletico kabla ya beki huyo kumuuma mwenzake kichwani ambaye alijitahidi kujinasua na kumshambulia mbaya wake na wote wakaonyeshwa kadi za njano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHEZAJI WA ATLETICO MADRID B AMNG'ATA WA REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top