• HABARI MPYA

    Friday, January 16, 2026

    NICKSON KIBABAGE AJIUNGA NA SIMBA SC BILA MALIPO


    BEKI wa kushoto, Nickson Clement Kibabage (25) amejiunga na klabu ya Simba SC akitokea Singida Black Stars kama mchezaji huru baada ya maridhiano ya pande zote mbili.
    Kibabage alijiunga tena na Singida Black Stars msimu huu akitokea Yanga alikodumu kwa misimu miwili kati ya mwaka 2023-2025.
    Alikwenda Yanga SC akitokea Singida Black Stars ambako awali alicheza kwa msimu mmoja akitokea KMC ambako alikuwa anacheza kwa mkopo kutoka Difaâ Hassani El Jadidi ya Morocco.
    Kibabage alijiunga na Difaâ Hassani El Jadidi mwaka 2019 akitokea Mtibwa Sugar iliyomuibua katika timu yake ya vijana na kufanya vizuri kikosi cha kwanza msimu mmoja tu, 2018-2019 kabla ya kuuzwa Morocco kwa mkataba wa miaka minne. 



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NICKSON KIBABAGE AJIUNGA NA SIMBA SC BILA MALIPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top