MAKAMBO, DJUMA SHABANI WAFUNGA PENALTI TABORA UNITED YAICHAPA NAMUNGO 2-1
TIMU ya Tabora United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mabao ya Tabora United yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Heritier Ma Olongi Makambo dakika 72 kwa penalti na beki mzawa, Salum Abdallah Chuku dakika ya 90'+2, wakati bao pekee la Namungo FC limefungwa na beki Mkongo, Djuma Shabani kwa penalti pia dakika ya 60. Ni ushindi wa kwanza katika mchezo wa pili ikitoka kufungwa 3-0 na Simba wiki iliyopita Dar es Salaam, wakati Namungo FC leo imecheza mechi yake ya kwanza ya msimu.
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment