KLABU ya Simba imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na Al Hilal Omdurman ya Sudan katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) Jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
Mshambuliaji mpya, Mcameroon Christian Leonel Ateba Mbida (25) alianza kuifungia Simba katika mechi yake ya kwanza tangu asajiliwe kutoka USM Alger ya Algeria dakika ya 25, kabla ya winga wa kushoto Muivory Coast, N'guessan Serge Archange Pokou kuisawazishia Hilal dakika ya 76.
Mchezo huo ulikuwa wa matayawisho kwa timu zote kujiandaa na mechi za Raundi ya Kwanza za michuano ya Afrika, A Hilal wakicheza Ligi ya Mabingwa na Simba Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba itakuwa mgeni wa Al Ahli Septemba 13 Uwanja wa Juni 11 Jijini Tripoli katika mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 20 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wao, Al Hilal watakuwa wageni wa San-Pédro FC Septemba 13 Uwanja wa Laurent Pokou Jijini San-Pedro, kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 20 Uwanja wa Juba Jijini Juba nchini Sudan.
0 comments:
Post a Comment