Tetesi za J'tano magazeti Ulaya

MAN CITY KARIBU KUMSAJILI STEVEN JOVETIC
Stevan Jovetic
Manchester City ipo karibu kufikia makubaliano na Fiorentina ya kumsajili mshambuliaji mwenye umri wa miaka 22-raia wa Montenegro, Stevan Jovetic katika klabu hiyo msimu ujao.
Kocha wa zamani wa Liverpool, Rafael Benitez alinyimwa fedha za kumsajili Jovetic mwaka 2009 wakati huo, klabu hiyo ilikuwa inamilikiwa na Tom Hicks na George Gillett. Katika kitabu chake kipya, Benitez amesema Wamarekani hao walishindwa kumsaidia kifedha na matokeo yake Liverpool wakashindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, wakimaliza nafasi ya pili.
Arsenal na Tottenham zinashindana kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Hispania, Adrian Lopez, ambaye dau lake ni pauni Milioni Milioni 14.4.
Liverpool inapigana vikumbo na Juventus kuwania saini na winga wa  Argentina, Luciano Vietto. Wasaka vipaji wa Wekundu hao wamekuwa wakimfuatilia kinda huyo wa miaka 18 wa Racing Club Avellaneda, kiungo mwenye thamani ya pauni Milioni 4.
Manchester United bado inampigia hesabu mshamuliaji wa Sassuolo, Domenico Berardi baada ya kinda huyo wa umri wa miaka 18 kuanza vizuri Ligi Daraja la Kwanza Italia, Serie B.

KESI YA JT SEPTEMBA 24

Chama cha Soka England kitaanza kusikiliza kesi ya ubaguzi ya John Terry, Septemba 24, baada ya kuchelewa kufanya kwa tume huru ya watau watatu, Kamisheni ya Taratibu Inayojitegemea.

MESSI AZOMEWA, RONALDO APAISHWA

Mashabiki wa Peru walimzomea Lionel Messi wakitaja jina la "Cristiano, Cristiano" - wakimaanisha wanamzimikia nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo - wakati mshambuliaji huyo wa Argentina alipowasili Uwanja wa Ndege wa Lima kwa ajili ya mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia.