Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya


MANCHESTER  CITY, MAN UNITED ZAMGOMBEA VAN PERSIE...


NAHODHA wa Arsenal, Robin van Persie ameamua kutosaini mkataba mpya na klabu yake hiyo na kwa sababu hiyo anaweza kufuata mshahara bwa pauni 220,000 kwa wiki katika klabu bingwa England, Manchester City.
KLABU ya Manchester United nayo imeonyesha nia ya kumsajili mfungaji bora wa Ligi Kuu ya England, Robin Van Persie, Mholanzi mwenye umri wa miaka 28 na wana matumaini makubwa watamdondoshea Old Trafford.
Mark Hateley amemtaka mshambuliaji wa Liverpool, Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23, kuondoka Liverpool na kujiunga na AC Milan, akisema kwamba kwa kufanya hivyo atakuwa mchezaji babu kubwa zaidi.
NYOTA wa Italia, Andrea Pirlo amemtaka mshambuliaji, Mario Balotelli, mwenye umri wa miaka 21, kujiunga naye katika klabu ya Juventus, baada ya kusema kwamba sasa anajua namna ya kumchezesha mchezaji huyo wa Manchester City ili apige mabao lukuki.
KLABU ya Sunderland imejiunga katika mbio za kuwania saini ya nyota wa Ajax, Vurnon Anita, kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Uholanzi. Newcastle tayari imeweka dau la pauni Milioni 4.5 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, lakini likapigwa chini.
NYOTA wa zamani wa Real Madrid, Guti, mwenye umri wa miaka 35, anafanya mazoezi na West Ham kuelekea kujiunga nayo kama mchezaji huru.
Anderson
Anderson anaweza kurejea Ureno
KLABU ya Benfica inamfukuzia kiungo wa Manchester United, Anderson, mwenye umri wa miaka 24, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ureno.
KLABU ya Newcastle United ipo karibu kuinasa saini ya beki wa kulia wa Lille ya Ufaransa, Mathieu Debuchy, mwenye umri wa miaka 26, licha ya Inter Milan ya Italia nayo kutuopa ndoana zake.
KLABU ya Fulham ipo tayari kumsaini kipa wa Blackburn, Paul Robinson, mwenye umri wa miaka 32, baada ya mpango wake wa kuhamia Besiktas kudunda.

DI MATTEO ATETEA BASI LAKE CHELSEA

KOCHA wa Chelsea, Roberto Di Matteo amesema ni makosa kuisema timu yake inakosea kwa staili yake ya kucheza kwa kupaki basi kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona katika Nusu Fainali na Bayern Munich katika fainali, ambazo zote walishinda na kutwaa ubingwa.

ARBEOLA APAGAWA...

BEKI wa Hispania, Alvaro Arbeloa alikuwa mwenye furaha kubwa mno wakati wa kushangilia ubingwa wa Euro 2012 na mashabiki nchini humo, kiasi cha kufikia kuruka kutoka kwneye basi.