• HABARI MPYA

    Monday, July 02, 2012

    TORRES ATWAA KIATU CHA DHAHABU


    MSHAMBULIAJI Fernando Torres, ametwaa tuzo ya mfungaji bora wa Euro 2012, Kiatu chja Dhahabu baada ya kufunga bao lake la tatu dhidi yas Italia usiku wa leo katika fainali.
    Hispania imekuwa bingwa kwa kushinda 4-0, akifungana na wachezaji wenzake watano
    Main man: Fernando Torres has won the Golden Boot at Euro 2012
    KIFAA: Torres ametwaa kiatu cha dhahabu Euro 2012

    WAFUNGAJI BORA EURO 2012

    MABAO MATATU...
    Fernando Torres (Hispania)
    Mario Gomez (Ujerumani)
    Alan Dzagoyev (Urusi)
    Mario Mandzukic (Croatia)
    Mario Balotelli (Italia)
    Cristiano Ronaldo (Ureno)
    Mechi pekee ambayo Torres alianza katika fainali hizi ilikuwa dhidi ya Ireland, ambayo alifunga mabao mawili.
    Alitolewa na nafasi yake akapewa Fabregas. 
    Torres pia alitoa mchango mkubwa kwa klabu yake, Chelsea kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akifunga kwenye Nusu Fainali dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi, Barcelona.
    Kumalizia kwake msimu vizuri, kulikuja baada ya kupitia kipindi kigumu katika Ligi Kuu.
    Kilichomuokoa ni kuteuliwa kwa Roberto Di Matteo kuwa kocha Mkuu kamili wa klabu na kuondoka kwa mshasmbuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba kuhamia China.
    Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ameweka wazi anamtaka Di Matteo kujenga safu ya ushambuliaji ya Mspanyola huyo, Eden Hazard na Marko Marin washirikiane na Mata.
    Baada ya mafanikio yake haya, tutarajie nini makubwa kutoka kwa Torres? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.



    Daddy's girl: Torres with his children after he helped Spain beat Italy
    Kabinti kake: Torres akishangilia na mtoto wake wa kike
    Daddy's girl: Torres with his children after he helped Spain beat Italy
    Daddy's girl: Torres with his children after he helped Spain beat Italy

    Chelsea connection: Torres celebrates with Juan Mata who scored Spain's fourth
    Wakali wa Chelsea: Torres akishangilia na Juan Mata aliyefunga bao la nne

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TORRES ATWAA KIATU CHA DHAHABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top