• HABARI MPYA

    Wednesday, July 08, 2026

    USWISI YAITOA COLOMBIA KWA MATUTA NA KUTINGA ROBO FAINALI


    TIMU ya Uswisi imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya bila mabao na Colombia ndani ya dakika 120 usiku wa huu Uwanja wa BC Place Jijini Vancouver nchini Canada. 
    Waliofunga penalty za Uswisi ni Granit Xhaka, Mohamed Amdouni, Cedric Itten na Rubén Vargas huku Manuel Akanji pekee akikosa, wakati kwa upande wa Colombia waliofunga ni Juan Quintero, Jaminton Campaz na Luis Díaz huku Davinson Sánchez na Juan Hernández wakikosa.
    Sasa Uswisi itakutana na Argentina Julai 11 Uwanja wa Arrowhead, Kansas City, Missouri, Marekani – wakati Robo Fainali nyingine ni Ufaransa na Morocco Julai 9 Uwanja wa Gillette, Foxborough, Massachusetts, Marekani, Hispania na Ubelgiji Julai 10 Uwanja wa SoFi, Inglewood, California, Marekani na Norway dhidi ya England Julai 11 pia Uwanja wa Hard Rock, Florida, Miami Gardens, Marekani.

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: USWISI YAITOA COLOMBIA KWA MATUTA NA KUTINGA ROBO FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top