• HABARI MPYA

  Monday, September 03, 2018

  ZAHERA AFUTA MECHI YA KIGOMA YANGA, TIMU YABAKI DAR KUJIANDAA NA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MECHI ya kirafiki baina ya Yanga SC na Singida United iliyopangwa kufanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma Jumatano imefutwa.
  Bin Zubeiry Sports – Online inafahamu kwamba uongozi wa Yanga uliandaa mechi hizo kwa lengo kukusanya fedha, lakini kocha Mkuu wa klabu, Mwinyi Zahera raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amekataa.
  Baada ya kuambiwa umbali wa kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma ambako kwa barabara ni siku mbili njiani kwenda na siku mbili kurudi, Zahera amefuta mechi hiyo na ile iliyotarajiwa kufanyika Sumbawanga pia. 

  Ndoto za mashabiki wa Yanga wa Kigoma kumuona nyota mpya wa timu yao, Mkongo Heritier Makambo zimeyeyuka

  Anataka kutumia muda huu kuiandaa timu yake kwa ajili ya mechi zijazo za Ligi Kuu, dhamira yake kubwa ikiwa ni kutwaa ubingwa wa. 
  Sasa kikosi cha Yanga kitaendelea na mazoezi Uwanja wa Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Polisi, Kurasini mjini Dar es Salaam.
  Mechi za Yanga za Ligi, pamoja na za Azam FC na Simba zimesimamishwa kupisha maandalizi ya mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kati ya Tanzania na Uganda Septemba 8 mjini Kampala.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZAHERA AFUTA MECHI YA KIGOMA YANGA, TIMU YABAKI DAR KUJIANDAA NA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top