• HABARI MPYA

    Sunday, September 02, 2018

    THOMAS ULIMWENGU AENDELEZA MOTO WA MABAO SUDAN, AFUNGA TENA AL HILAL YASHINDA 4-0

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu usiku wa Jumamosi ameifungia klabu yake, Al Hilal Omdurman katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Al Khartoum kwenye Ligi Kuu ya Sudan.
    Sasa, Ulimwengu anarejea nyumbani kujiunga na timu yake ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa ugenini kufuzu AFCON dhidi ya Uganda Septemba 8 mjini Kampala.
    Ulimwengu aliyejiunga na El HIlal Juni mwaka huu ni miongoni mwa nyota tisa wanaocheza nje walioitwa na kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa wiki ijayo Uwanja wa Mandemla mjini Kampala.

    Thomas Ulimwengu (kushoto) ameifungia Al Hilal ikishinda 4-0 dhidi ya Al Khartoum kwenye Ligi Kuu ya Sudan PICHA YA MAKTABA

    Wengine ni mabeki Hassan Kessy wa Nkana FC ya Zambia, Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini, viungo, Himid Mao wa Petrojet ya Misri, Simon Msuva wa Difaa Hassan El-Jadida, Morocco, Farid Mussa na washambuliaji Shaaba Iddi wa CD Tenerife ya Hispania, Rashid Mandawa wa BDF XI ya Botswana na Nahodha Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji.
    Wachezaji wengine waliopo kambini Taifa Stars ni makipa Aishi Manula wa Simba SC, Benno Kakolanya wa Yanga SC na Mohammed Abdulrahman Wawesha wa JKU, mabeki David Mwantika wa Azam FC, Ally Sonso, Paul Ngalema wa Lipuli FC ya Iringa, Gardiel Michael, Kelvin Yondan na Andrew Vincent ‘Dante’ wa Yanga SC, Aggrey Morris.
    Viungo ni Salum Kimenya wa Tanzania Prisons ya Mbeya, Frank Domayo wa Azam FC, Salum Kihimbwa wa Mtibwa Sugar, Mudathir Yahya na washambuliaji Yahya Zayed wa Azam FC na Kelvin Sabato wa Mtibwa Sugar. 
    Taifa Stars iliingia kambini Jumanne wiki hii katika hoteli ya Sea Scape, eneo la Kunduchi mjini Dar es Salaam na inafanya mazoezi Uwanja wa Boko Veterani.
    Wachezaji wengine waliopo kambini TaifaStars ni makipa Aishi Manula wa Simba SC, Benno Kakolanya wa Yanga SC na Mohammed Abdulrahman Wawesha wa JKU, mabeki Gardiel Michael, Kelvin Yondan na Andrew Vincent ‘Dante’ wa Yanga SC, Aggrey Morris, kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Yahya Zayed wa Azam FC.
    Amunike aliyesaini mkataba wa kufundisha Taifa Stars mapema Agosti, ambaye anasaidiwa na Mnigeria mwenzake, Emeka Amadi na Mzalendo, Hemed Suleiman ‘Morocco’, baada ya mechi na Uganda Septemba 8, mwaka huu mjini Kampala, atawafuata Cape Verde Oktoba 10 kukamilisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
    Na hiyo ni baada ya Taifa Stars kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Lesotho Juni 10, mwaka jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam ikiwa chini ya kocha mzalendo, Salum Mayanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: THOMAS ULIMWENGU AENDELEZA MOTO WA MABAO SUDAN, AFUNGA TENA AL HILAL YASHINDA 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top