• HABARI MPYA

    Sunday, January 04, 2026

    TAIFA STARS YATOLEWA AFCON, YACHAPWA 1-0 NA MOROCCO, ILA REFA…


    SAFARI ya Tanzania katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 imeishia Hatua ya 16 Bora baada ya kutolewa na wenyeji, Morocco leo.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah Jijini Rabat, bao pekee la Simba wa Atlasi limefungwa na winga wa Real Madrid ya Hispania, Brahim Abdelkader Díaz dakika ya 64.
    Kocha wa Tanzania, Muargentina Miguel Angel Gamondi na wachezaji wake walimlalamikia refa Boubou Traore wa Mali kuwanyima penalti kufuatia winga Iddi Suleiman ‘Nado’ kuangushwa kwenye boksi dakika ya 90 na ushei.
    Morocco sasa itakutana na mshindi kati ya Afrika Kusini na Cameroon zitakazomenyana baadaye usiku huu Uwanja wa Al Medina hapo hapo Rabat.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS YATOLEWA AFCON, YACHAPWA 1-0 NA MOROCCO, ILA REFA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top