TIMU ya Simba SC ya Dar es Salaam imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwembe Makumbi City FC katika mchezo wa Kundi B usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, winga Mkenya Mohammed Omar Ali Bajaber dakika ya 22 na sasa Simba watahitaji ushindi kwenye mchezo wao wa mwisho wa Kundi hilo dhidi ya Fufuni FC ya Pemba Jumatatu ili kujikatia tiketi ya Nusu Fainali.



.png)
0 comments:
Post a Comment