• HABARI MPYA

    Friday, January 02, 2026

    AZAM FC YAWACHAPA MLANDEGE SC 2-0 KOMBE LA MAPINDUZI


    MABAO ya viungo Zidane Ally Sereri dakika ya tano na Himid Mao Mkami dakika ya 54 yameipa Azam FC ushindi wa 2-0 dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi, Mlandege FC katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Azam FC inafikisha pointi nne baada ya ushindi huo kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 na Singida Black Stars katika mchezo wa kwanza hapo hapo Amaan Complex.
    Mlandege inakamilisha mechi zake tatu za Kundi A kwa kufungwa zote, nyingine 3-1 na Singida Black Stars na 1-0 na URA FC ya Uganda.
    Sasa timu za Azam FC na Singida Black Stars zitahitaji kushinda dhidi ya URA ili kupata tiketi ya kwenda Nusu Fainali. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAWACHAPA MLANDEGE SC 2-0 KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top