• HABARI MPYA

    Saturday, March 29, 2025

    MABINGWA WATETEZI, YANGA NAO WATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CRDB


    MABINGWA watetezi, Yanga wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Songea United jioni ya Leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
    Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo Mkenya, Duke Ooga Abuya dakika ya 22 na winga Mkongo, Jonathan Ikangalombo dakika ya 54 wote wakimalizia kazi nzuri za kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MABINGWA WATETEZI, YANGA NAO WATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CRDB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top