TIMU ya JKT Tanzania imefanikiwa kuingia Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya Kwanza jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Beki Ibrahim Ngecha alijifunga dakika ya 10 tu kuipatia bao la kuongoza JKT Tanzania, kabla ya mshambuliaji Edward Songo kufunga mawili dakika ya 14 na 17 kuhitimisha shangwe za mabao za timu ya Jeshi la Kujenga Taifa.
Nayo Singida Black Stars imetinga Robo Fainali pia baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya KMC leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.
Mechi nyingine ya 16 Bora Kombe la CRDB leo Mbeya City imeitupa nje Mtibwa Sugar kwa kuichapa 2-1 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
0 comments:
Post a Comment