BAO pekee la mshambuliaji Mghana, Jonathan Sowah dakika ya 79 limeipa Singida Black Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 44, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 23, nayo inabaki nafasi ya 12 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 23 sasa.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment