// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SERENGETI GIRLS YATANDIKWA 3-0 NA ZAMBIA KIFUZU KOMBE LA DUNIA U17 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SERENGETI GIRLS YATANDIKWA 3-0 NA ZAMBIA KIFUZU KOMBE LA DUNIA U17 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 09, 2025

    SERENGETI GIRLS YATANDIKWA 3-0 NA ZAMBIA KIFUZU KOMBE LA DUNIA U17


    TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls imefungwa mabao 3-0 na Zambia katika mchezo wa kwanza Raundui ya Pili kufuzu Fainali za Kombe la Dunia leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.  
    Mabao ya Zambia ‘Copper Princesses’ yamefungwa na Grace Phiri dakika ya 64 na Mercy Chipasula mawili, dakika ya 80 na 89  kwa penalti.
    Timu hizo zitarudiana Machi 15 Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Benin na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika raundi ya Tatu na ya mwisho ya kuwania tiketi ya Fainali za Dunia zitakazofanyika nchini Morocco kuanzia Oktoba 17 hadi Novemba 8, mwaka huu.
    Mwaka jana Serengeti Girs ilitolewa na pia na Copper Princesses katika hatua kama hii ya kufuzu Kombe la Dunia kwa kuchapwa 5-0 Lusaka Februari 3, kabla ya kushinda 1-0 Dar es Salaam hapo hapo Chamazi Februari 11.
    Ikumbukwe Serengeti Girls ni timu pekee ya soka Tanzania iliyowahi kucheza Fainali za Kombe la Dunia – ilikuwa mwaka 2022 nchini India ambako ilifika hadi Robo Fainali na kutolewa na Colombia kwa kuchapwa 3-0.
    Katika Kundi lake ilishinda 2-1 dhidi ya Ufaransa, kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Canada kufuatia kufungwa 4-0 na Japan katika mchezo wa kwanza – hivyo kumaliza na pointi nafasi ya pili nyuma ya Japan iliyomaliza na pointi tisa na wote kufuzu Robo Fainali.
    Kwa upande wao, Canada walimaliza na pointi mbili ya tatu na Ufaransa waliomaliza na pointi moja wakashika mkia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI GIRLS YATANDIKWA 3-0 NA ZAMBIA KIFUZU KOMBE LA DUNIA U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top