TIMU ya Norway imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Dunia baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brazil usiku wa kuamkia leo Uwanja wa MetLife Jijini East Rutherford, New Jersey, New York, Marekani.
Mabao yote ya Norway katika mchezo huo yamefungwa na mshambuliaji wa Manchester City ya England, Erling Braut Haaland dakika ya 79 na 90 huku bao la kufutia machozi la Brazil likifungwa na mshambuliaji wa Santos ya kwao, Neymar da Silva Santos Júnior kwa penalti dakika ya 90’+10.
Kwa matoleo hayo, Norway itakutana na mshindi kati ya Mexico na England katika Robo Fainali Julai 5 Uwanja wa Azteca Jijini Mexico City nchini Mexico.



.png)
0 comments:
Post a Comment