TIMU ya Ivory Coast imeanza vyema Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ecuador katika mchezo wa Kundi F usiku wa Jumapili Uwanja Lincoln Financial Field, Philadelphia, Pennsylvania, Marekani.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, winga wa Manchester United ya England, Amad Diallo dakika ya 90 na kuifanya Ivory Coast kuwa timu ya kwanza ya Afrika kushinda mechi kwenye Fainali za mwaka huu.
Ikumbukwe kwenye mchezo mwingine wa Kundi E jana Ujerumani nayo ilianza kwa kishindo baada ya kuitandika Curaçao mabao 7-1 Uwanja wa NRG Jijini Houston, Kusini mwa Marekani.



.png)
0 comments:
Post a Comment