• HABARI MPYA

  Saturday, September 01, 2018

  MOUSSA DEMBELE ATUA UFARANSA KWA PAUNI MILIONI 22

  KLABU ya Lyon ya Ufaransa imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Moussa Dembele kutoka Celtic dau la Pauni Milioni 22. 
  Dembele, mshambuliaji mwenye kasi mwenye umri wa miaka 21, amefunga mabao 51 katika mechi 94 katika klabu hiyo ya Jiji la Glasgow.
  Nayo PSG imetangaza kumsajili mshambuliaji Mcameroon, Eric Maxim Choupo-Moting muda mfupi kabla ya kufungwa dirisha la usajili kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Stoke City kwa dau la Pauni Milioni 13.5. 

  Moussa Dembele amejiunga na Lyon kutoka Celtic dau la Pauni Milioni 22 

  Choupo-Moting alicheza chini ya Tuchel kwa misimu mitatu katika klabu ya Mainz ya Ujerumani kuanzia mwaka 2011 hadi 2014.
  Ameifungia mabao 32 Stoke City, lakini hajacheza tena tangu iangukie Championship kutoka Ligi Kuu katikati ya mwaka huu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOUSSA DEMBELE ATUA UFARANSA KWA PAUNI MILIONI 22 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top