• HABARI MPYA

    Saturday, September 01, 2018

    HIMID MAO AWASHIKA MISRI, AISAIDIA PETROJET KUVUNA POINTI SABA KATIKA LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami, usiku wa jana amecheza dakika zote 90, timu yake, Petrojet ikilazimishwa sare ya 0-0 na Haras El Hodood katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri Uwanja wa Suez, As-Suways mjini Suez.
    Baada ya mechi ya tano ya msimu, Petrojet wakivuna pointi sana na kuangukia nafasi ya saba, Himid atapanda ndege kurejea nyumbani kuchezea timu yake ya taifa mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Uganda Septemba 8 mjini Kampala.
    Mao aliyejiunga na Petrojet Juni mwaka huu ni miongoni mwa nyota tisa wanaocheza nje walioitwa na kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa wiki ijayo Uwanja wa Mandemla mjini Kampala.

    Himid Mao (kushoto) jana amecheza dakika zote 90, timu yake, Petrojet ikilazimishwa sare ya 0-0 na Haras El Hodood

    Wengine ni mabeki Hassan Kessy wa Nkana FC ya Zambia, Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini, viungo, Simon Msuva wa Difaa Hassan El-Jadida, Morocco, Farid Mussa na washambuliaji Shaaba Iddi wa CD Tenerife ya Hispania, Rashid Mandawa wa BDF XI ya Botswana, Emmanuel Ulimwengu wa El HIlal ya Sudan na Nahodha Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji.
    Wachezaji wengine waliopo kambini Taifa Stars ni makipa Aishi Manula wa Simba SC, Benno Kakolanya wa Yanga SC na Mohammed Abdulrahman Wawesha wa JKU, mabeki David Mwantika wa Azam FC, Ally Sonso, Paul Ngalema wa Lipuli FC ya Iringa, Gardiel Michael, Kelvin Yondan na Andrew Vincent ‘Dante’ wa Yanga SC, Aggrey Morris.
    Viungo ni Salum Kimenya wa Tanzania Prisons ya Mbeya, Frank Domayo wa Azam FC, Salum Kihimbwa wa Mtibwa Sugar, Mudathir Yahya na washambuliaji Yahya Zayed wa Azam FC na Kelvin Sabato wa Mtibwa Sugar. 

    Amunike aliyesaini mkataba wa kufundisha Taifa Stars mapema Agosti, ambaye anasaidiwa na Mnigeria mwenzake, Emeka Amadi na Mzalendo, Hemed Suleiman ‘Morocco’, baada ya mechi na Uganda Septemba 8, mwaka huu mjini Kampala, atawafuata Cape Verde Oktoba 10 kukamilisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
    Na hiyo ni baada ya Taifa Stars kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Lesotho Juni 10, mwaka jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam ikiwa chini ya kocha mzalendo, Salum Mayanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HIMID MAO AWASHIKA MISRI, AISAIDIA PETROJET KUVUNA POINTI SABA KATIKA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top