KLABU ya Mbeya City imemtambulisha kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Yacouba Songne kuwa mchezaji wake mpya kuanzia dirisha hili dogo.
Yacouba Songné anajiunga na Mbeya City baada ya kuachana na iliyokuwa Tabora United, sasa TRA United ambayo aliichezea msimu uliopita akitokea AS Arta/Solar7 ya Djibouti.
Yacouba Songné aliwasili nchini kwa mara ya kwanza Agosti mwaka 2020 kujiunga na Yanga SC akitokea Asante Kotoko ya Ghana baada ya awali kuchezea Stade Malien ya Mali kufuatia kuchezea klabu mbili za kwao, Burkina Faso, RC Kadiogo na
EF Ouagadougou.
Baada ya kuondoka Yanga, Yacouba Songné alichezea Ihefu SC ambayo sasa inajulikana kama Singida Black Stars.



.png)
0 comments:
Post a Comment