• HABARI MPYA

  Wednesday, September 19, 2018

  MAKAMBO AIPELEKA YANGA SC KILELENI LIGI KUU, YAIPIGA COASTAL UNION 1-0 UWANJA WA TAIFA

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi ya wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Heritier Makambo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na sasa Yanga SC inafikisha pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu na zote nyumbani, nyingine 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro na 4-3 dhidi ya Stand United ya Shinyanga.   
  Yanga SC sasa wanaongoza Ligi Kuu kwa wastani wa mabao tu, kwani kwa pointi wanalingana na JKT Tanzania ilityocheza mechi moja zaidi, wote wakifuatiwa na Azam FC yenye point inane za mechi nne na Simba SC, mabingwa watetezi wenye pointi saba ambao kesho watacheza mechi yao ya nne dhidi ya Mbao FC mjini Mwanza.
  Kipa Klaus Kindoki akimpongeza Mkongo mwenzake, Heritier Makambo baada ya kufunga bao pekee leo 
  Mapema dakika ya pili Heritier Makambo alipiga kichwa mpira ukatoka nje kidogo ya lango  
  Kiungo Deus Kaseke akijaribu kumpita beki wa Coastal Union  
  Kiungo Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi akipambana na wachezaji wa Coastal Union
    
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abubakari Mturo kutoka Mtwara, aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Charles Simon wa Dodoma, Makambo alifunga bao hilo dakika ya 11 kwa guu lake la kulia akimalizia ‘majaro’ ya Ibrahim Ajib.
  Yanga SC ilipatwa na uchu wa mabao zaidi baada ya bao hilo, lakini wakaishia kupoteza nafasi walizotengeneza huku Coastal Union nao wakiishia kulitia misukosuko tu lango la wenyeji lililouwa linalindwa na kipa Mkongo, Klaus Kindoki.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Klaus Kindoki, Paulo Nyanganya, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Mrisho Ngassa/Matheo Anthony dk58, Papy Kabamba Tshishimbi, Heritier Makambo/Amissi Tambwe dk67, Ibrahim Ajib na Deus Kaseke/Ninjaa 75.
  Coastal Union; Hussein Sharrif 'Casillas', Mbwana Khamis ‘Kibacha’, Adeyum Ahmed, Ibrahim Mohamed, Bakari Mwamnyeto, Hassan Hamisi, Issa Said, Athumani Iddi ‘Chuji’/Mtende Albano dk46, Hamisi Kanduru/MosesKitandu dk79, Andrew Simchimba na Ayoub Lyanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKAMBO AIPELEKA YANGA SC KILELENI LIGI KUU, YAIPIGA COASTAL UNION 1-0 UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top