• HABARI MPYA

    Friday, December 19, 2025

    STEVE BARKER NDIYE KOCHA MPYA SIMBA SC


    KLABU ya Simba SC imemtambulisha Steven Robert ‘Steve’ Barker (57) kuwa Kocha wake mpya Mkuu akichukua nafasi ya Mbulgaria, Dimitar Nikolaev Pantev aliyedumu kazini mwezi mmoja tu.
    Kama ilivyo kwa makocha wengi huanzia kwenye uchezaji, Steve Barker naye amechezea Wits University kuanzia mwaka 1990 hadi 1998 na SuperSport United kati ya mwaka 1999 na 2000, kabla ya kugeukia ukufunzi.
    Amefundisha klabu za University of Pretoria kuanzia mwaka 2008 hadi 2014 alipohamia AmaZulu ambako alifundisha hadi 2016 akaenda Stellenbosch mwaka.
    Simba inajaribu kupata kocha wa kuamini baada ya kuondoka kwa kocha wake mwingine raia wa Afrika Kusini Fadlu Davids aliyefanya kazi kwa mafanikio msimu uliopita.
    Baada ya kuifikisha Simba Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka jana na kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara katika siku ya mwisho akifungwa 2-0 na mtani, Yan has — Fadlu alitarajiwa kufanya zaidi msimu huu.
    Hata hivyo, baada ya mwezi mmoja ndani ya msimu mpya akaamua kuondoka kwenda kujiunga na Raja Athletic ya Morocco, maarufu kama Raja Casablanca ndipo Simba is kamchukua Pantev.
    Simba ilichana na Mbulgaria huyo kutokana na mwanzo mbaya katika mechi zake mbili za Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika ikifungwa nyumbani na ugenini.
    Simba SC ilifungwa 1-0 na Angola Petro de Luanda ya Angola katika mchezo wa kwanza Novemba 23 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya kufungwa 2-1 na Stade Malien Novemba 30 Uwanja wa Machi 26 Jijini Bamako nchini Mali. 
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STEVE BARKER NDIYE KOCHA MPYA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top