• HABARI MPYA

    Tuesday, December 16, 2025

    WATATU WANAOCHEZA ULAYA WARIPOTI KAMBINI TAIFA STARS CAIRO


    WACHEZAJI watatu zaidi wanaocheza nje wamewasili Jijini Cairo nchini Misri kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zinazotarajiwa kufanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21 hadi Januari 18, mwakani.
    Hao ni beki wa Salford City F.C. ya England, Haji Suleiman Haji Ali Mnoga na viungo, Tarryn Allarakhia wa Rochdale FC ya England na Novatus Dismas Miroshi wa Gotzepe ya Uturuki.
    Baada ya kuwasili kwa nyota hao, sasa wanasubiriwa wakongwe tu, Simon Happygod Msuva wa Al Talaba ya Iraq na Nahodha, Mbwana Ally Samatta wa Le Hevre ya Ufaransa, wote washambuliaji.
    Taifa Stars imeweka kambi nchini Misri kujiandaa na AFCON hadi Desemba 18 itakapoondoka kwenda Morocco tayari kwa Fainali hizo hizo za 35 za Kombe la Mataifa ya Afrika.



    Taifa Stars ambayo inashiriki Fainali hizo kwa mara ya nne baada ya 1980 Nigeria, 2019 Misri na 2023 Ivory Coast — imepangwa Kundi C pamoja na Nigeria, Tunisia na Uganda.
    Katika Fainali zote zilizotangulia Taifa Stars imekuwa ikitolewa hatua ya makundi - tena bila kushinda mechi hata moja wakitoa sare na kufungwa.
    Mwaka 1980 walifungwa 3-1 na Nigeria na 2-1 na Misri pamoja na Sara ya 1-1 na Ivory Coast, 2019 walifungwa mechi zote, 2-0 na Senegal, 3-2 na Kenya na 3-0 na Algeria — wakati mwaka 2023 walifungwa mechi moja, 3-0 na Morocco na sare za 1-1 na Zambia na 0-0 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WATATU WANAOCHEZA ULAYA WARIPOTI KAMBINI TAIFA STARS CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top