• HABARI MPYA

    Monday, December 15, 2025

    REAL MADRID YAICHAPA ALAVES 2-1 LA LIGA


    TIMU ya Real Madrid jana ilijiweka sawa kwenye mbio ubinga baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Deportivo Alavés katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Mendizorroza mjini Vitoria-Gasteiz, Álava.
    Mabao ya Real Madrid yalifungwa na mshambuliaji Mfaransa, Kylian Mbappé Lottin mwenye asili ya Cameroon dakika ya 24 na winga Mbrazil, Rodrygo Silva de Goes dakika ya 76, wakati bao pekee la Alaves lilifungwa na winga pia, Mspaniola Carlos Vicente Robles dakika ya 68.
    Kwa ushindi huo, Real Madrid inafikisha pointi 39, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nne na vinara, Barcelona baada ya timu zote kucheza mechi 17.
    Kwa upande wao Alaves ambao jana huo ulikuwa mchezo wa 16 wa msimu wa La Liga, wanabaki na pointi zao 18 nafasi ya 12 kwenye ligi ya timu 20.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REAL MADRID YAICHAPA ALAVES 2-1 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top