• HABARI MPYA

    Sunday, March 29, 2026

    TANZANIA YAIBAMIZA MACAU 6-0 MICHUANO YA FIFA YA FIFA SERIES RWANDA


    TIMU ya Tanzania imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Macau katika mchezo wa Kundi B kuwania nafasi tatu michuano ya FIFA Series jioni ya leo Uwanja wa Pele Jijini Kigali, Rwanda.
    Mabao ya Taifa Stars yamefungwa na mshambuliaji wa Floriana ya Malta, Kokola Charles William M'Mombwa dakika ya 16, nyota wa Yanga SC, beki Bakari Nondo Mwamnyeto dakika ya 26 na kiungo Mudathir Yahya Abbas dakika ya 45.
    Mengine yamefungwa na mshambuliaji wa JKT Tanzania, Paul Peter Kasunda dakika ya 56, kiungo wa Gotzepe ya Uturuki, Novatus Dismas Miroshi dakika ya 74 na winga wa Rochdale ya England, Tarryn Allarakhia dakika ya 87.
    Taifa Stars imeangukia kwenye mchezo wa kuwania nafasi ya tatu michuano ya FIFA ya Series mwaka huu baada kufungwa 1-0 na Liechtenstein katika mchezo wa kwanza Alhamisi hapo hapo Uwanja wa Pele.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA YAIBAMIZA MACAU 6-0 MICHUANO YA FIFA YA FIFA SERIES RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top