• HABARI MPYA

    Sunday, March 22, 2026

    SIMBA SC YANG'ARA LIGI KUU, YAICHAPA TRA UNITED 3-0 MBWENI


    TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
    Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Suleiman Abdallah Mwalimu dakika ya 12 kwa penalti na viungo, Neo Maema raia wa Afrika Kusini dakika ya 67 na mzawa, Yusuphu Ally Kagoma dakika ya 88.
    Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 14 na kupanda nafasi ya pili nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 38 na mechi mbili zaidi za kucheza.
    Kwa upande wao TRA United baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 20 za mechi 16 sasa nafasi ya 10 kwenye Ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YANG'ARA LIGI KUU, YAICHAPA TRA UNITED 3-0 MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top