TANZANIA imefungwa bao 1-0 na Liechtenstein katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kundi B michuano ya FIFA Series jioni ya leo Uwanja wa Pele Jijini Kigali nchini Rwanda.
Bao pekee la Liechtenstein limefungwa na winga, Ferhat Sağlam
wa Eintracht Hohkeppel inayoshiriki Ligi ya Ridhaa Daraja la Tano Ujerumani ijulikanayo kama Mittelrheinliga dakika ya 56.
Mapema katika mchezo uliotangulia mchana Aruba iliichapa Macau 4-1 hapo hapo Uwanja wa Pele Jijini Kigali.
Sasa Taifa Stars itakamilisha michuano hiyo Jumapili kwa kucheza na Macau Jumapili kuwania nafasi ya tatu ya kundi lake, wakati Liechtenstein itamenyana na Aruba katika Fainali kwa Kundi B.



.png)
0 comments:
Post a Comment