• HABARI MPYA

    Thursday, March 19, 2026

    AZAM FC YAAMBULIA SULUHU KWA MASHUJAA, 0-0 KIGOMA


    TIMU ya Azam FC imetoa sare ya 0-0 na wenyeji Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
    Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 29 ikisalia nafasi ya pili nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 37 baada ya timu zote kucheza mechi 15.
    Kwa upande wao Mashujaa baada ya sare ya leo wanafikisha pointi 19 katika mchezo wa 17 ilisalia pia nafasi ya 11.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAAMBULIA SULUHU KWA MASHUJAA, 0-0 KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top