• HABARI MPYA

    Wednesday, February 11, 2026

    SINGIDA BLACK STARS YAICHAPA FOUNTAIN GATE 1-0 CHAMAZI


    TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. 
    Bao pekee la Singida Black Stars katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo Mkongo, Linda Mtange dakika ya 64.
    Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 12 katika mchezo wa nane na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 13 ikiizidi tu wastani wa mabao Fountain Gate inayohamia nafasi ya 14.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BLACK STARS YAICHAPA FOUNTAIN GATE 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top