• HABARI MPYA

    Sunday, February 22, 2026

    SIMBA SC YAICHAPA TANZANIA PRISONS 2-0 DODMA

    TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
    Mabao ya  Simba SC leo yamefungwa na mshambuliaji mzawa, Suleiman Abdallah Mwalimu dakika ya 19 na beki wa kati raia wa Afrika Kusini, Rushine De Reuck kwa penalti dakika ya 45.
    Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 22 katika mchezo wa tisa na kusogea nafasi ya nne, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 12 za mechi 14 sasa nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16. 
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.  

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA TANZANIA PRISONS 2-0 DODMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top