TIMU ya Pamba Jiji FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mabao ya Pamba Jiji FC yamefungwa na kiungo Mrundi, Shassiri Nahimana mawili, dakika ya 71 na 76 na mshambuliaji Mkenya, Mathew Tegisi dakika ya 90.
Kwa ushindi huo, Pamba Jiji inafikisha pointi 20 katika mchezo Wa 13 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya tatu, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 11 za mechi 13 sasa nafasi ya 12 kwenye ligi ya timu 16.



.png)
0 comments:
Post a Comment