• HABARI MPYA

    Sunday, February 08, 2026

    SINGIDA BLACK STARS YAUMALIZA MWENDO KOMBE LA SHIRIKISHO


    MATUMAINI ya Singida Black Stars kwenda Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika yamezidi kufifia baada ya kuchapwa bao 1-0 na CR Belouizdad ya Algeria katika mchezo wa Kundi C usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. 
    Bao pekee la CR Belouizdad katika mchezo huo limefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Algeria, Abdennour Iheb Belhocini dakika ya tatu tu ya mchezo huo.
    Kwa ushindi huo, CR Belouizdad inafikisha pointi 12 kileleni mwa kundi hilo na kuhihakikishia tiketi ya Robo Fainali, wakati Singida Black Stars inabaki na pointi zake nne na kupoteza kabisa nafasi ya kwenda Robo Fainali baada ya mechi za Raundi ya tano.
    AS Otohô ya Jamhuri ya Kongo imejikatia tiketi ya Robo Fainali pia baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stellenbosch Uwanja Wa Alphonse Massemba-Débat Jijini Brazzaville na kufikisha pointi tisa katika nafasi ya pili.
    As Otoho itamaliza ugenini dhidi ya CR Belouizdad Uwanja wa Nelson Mandela Jijini Algiers, wakati Singida Black Stars inakwenda Afrika Kusini kumenyana na Stellenbosch Uwanja wa Cape Town Jijini Cape Town.
    Zote, Singida Black Stars na Stellenbosch zimevuna pointi nne kila moja katika mechi tano. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BLACK STARS YAUMALIZA MWENDO KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top