TIMU ya Dodoma Jiji FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TRA United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na mshambuliaji Faraji Kayanda dakika ya 15, beki Gardiel Michael dakika ya 40 na mshambuliaji, William Edgar dakika ya 55.
Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 15 na kusogea nafasi ya sita, wakati TRA United inabaki na pointi zake 13 za mechi 12 nafasi ya 11 kwenye ligi ya timu 16.


.png)
0 comments:
Post a Comment