TIMU ya Morocco imeendelea kuliwakilisha vyema Bara la Afrika katika michuano ya Kombe la Dunia baada ya kufanikiwa kwenda Hatua ya Robo Fainali kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wenza, Canada usiku huu katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Uwanja wa NRG Jijini Houston, Texas nchini Marekani.
Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza – kiungo wa Girona ya Hispania, Azzedine Ounahi alifunga mabao mawili dakika ya 50 na 82, kabla ya mshambuliaji wa Al Ain ya Falme za Kiarabu (UAE), Soufiane Rahimi kufunga la tatu dakika ya 90’+8.
Ushindi huo unamaanisha Morocco inakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuingia Robo Fainali ya Kombe la Dunia mara mbili, tena mfululizo na sasa itakutana na mshindi kati ya Paraguay na Ufaransa zinanzomenyana baadaye usiku huu.
Ikumbukwe Morocco pia ndio wanashikilia rekodi ya timu ya Afrika iliyowahi kufika mbali zaidi kwenye michuano hiyo, Nusu Fainali hatua ambayo walifika katika Fainali zilizopita zilizofanyika nchini Qatar mwaka 2022.



.png)
0 comments:
Post a Comment