• HABARI MPYA

  Thursday, September 20, 2018

  SAMATTA AFUNGA BAO TAMU LA PILI KRC GENK YASHINDA 2-0 MICHUANO YA EUROPA LEAGUE

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo amefunga bao la pili timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Malmo FF ya Sweden katika mchezo wa Kundi L Europa League.
  Samatta alifunga bao hilo dakika ya 71 Uwanja wa Luminus Arena, baada ya mshambuliaji kinda wa umri wa miaka 23, Leandro Trossard kufunga bao la kwanza dakika ya 37.
  Na Samatta ambaye Desemba 13 atatimiza miaka 26 leo amefikisha mabao 29 aliyofunga kwenye mechi za mashindano tangu ajiunge na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Mbwana Samatta akishangilia baada ya kuifungia KRC Genk katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Malmo FF. Picha ya chini anapongezwa na wenzake 

  Ikumbukwe Mazembe ilikuwa klabu ya tatu ya ngazi ya Ligi Kuu kwa Samatta baada ya African Lyon aliyopanda nayo kutoka Daraja la Kwanza na SImba SC, zote za Dar es Salaam nchini Tanzania.  
  Samatta anatarajiwa kuiongoza tena Genk katika mchezo wa ugenini wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Jumamosi dhidi ya Cercle Brugge Uwanja wa Jan Breydelstadion mjini Brugge.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vukovic, Uronen, Dewaest, Aidoo, Maehle, Berge, Malinovskyi, Pozuelo/Seck dk75, Trossard, Samatta/Ingvartsen dk85 na Ndongala/Paintsil dk71.
  Malmo FF : Dahlin, Safari/Binaku dk79, Rieks, Lewicki, Bachirou, Rosenberg, Christiansen, Bengtsson, Antonsson/Traustason dk54, Nielsen na Vindheim.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AFUNGA BAO TAMU LA PILI KRC GENK YASHINDA 2-0 MICHUANO YA EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top